Afisa wa polisi mwenye cheo cha koplo amekutwa amekufa asubuhi ya usiku aliyokuwa zamu katika uwanja wa Jomo Kenyatta International Airport (JKIA).
Kwa jina anaitwa Gaudencia Wausi (28) na alikutwa amejipiga risasi kichwani msalani asubuhi ya Agosti 24, wakati akiwa zamu katika uwanja huo wa ndege
Ujumbe aliyouacha Afisa huyo wa polisi aliyejiua JKIA katika mtandao wa kijamii wa Facebook masaa matano kabla ya kifo chake, uliashiria kwamba marehemu alikua na mawazo ya kujiua. na ujumbe mwingine aliacha ulimhusu zaidi mwanaye wa kiume
“Mwanangu mpendwa, nakuombea ukue vizuri na Baraka. Nakuomba ukumbuke mie mamako nakupenda,” aliandika.
Mwili wa marehemu uligundulika na mfanyakazi wa usafi wa asubuhi saa mbili asubuhi katika uwanja huo, siku ya Jumatano, Agosti 24, 2016.
No comments:
Post a Comment