March 22, 2018

Mmiliki wa Facebook ameomba radhi kwa watumiaji wote wa mtandao huo

Mwanzilishi wa mtandao maarufu duniani wa Facebook, Mark Zuckerberg, kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica, inayotuhumiwa kuingilia data za watumiaji milioni 50 wa  mtandao huo, ameibuka na kudai kwamba wamefanya makosa.

Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zuckerberg bila kuomba radhi kwa kile kilichotokea, amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu. Hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa wala kudukuliwa kwa taarifa za watumiaji wake.

“Tuna wajibu wa kuzilinda taarifa zenu na kama tukishindwa kuzilinda hatuna sifa ya kuwahudumia, mimi ndiye niliyeanzisha mtandao huu wa Facebook, mwisho wa siku ninawajibika kwa chochote kinachotokea katika mtandao wetu,” amesema Zuckerberg.

Katika kufuatilia matatizo ya sasa na ya zamani amesema atafanya mambo yafuatayo;
  1.  Kuchunguza mitandao yote ambayo inashirikiana na uga wa Facebook kabla ya kufanyiwa mabadiliko ya mwaka 2014 ya namna ya kuweza kupata taarifa ya watumiaji.
  2. Kufanyia uchunguzi kazi za programu za kimitandao zinazotiliwa shaka.
  3. Kupiga marufuku mwanzilishi wa programu yoyote ambayo inagoma ama haitoi ushirikiano katika uchunguzi pamoja na hatua nyingine ambazo wanaona zitafanya Facebook kuwa mahali salama.

No comments:

Post a Comment