August 26, 2016

Polisi Yakabiliana na Majambazi, Mkuranga

bunduki
bunduki
Add caption

Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.
Magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.
Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkuranga, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru  zimefungwa kutokana na mapambano hayo.
Aidha taarifa za awali ziliripoti kuwepo na majibizano ya risasi kati ya jeshi la Polisi na watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi maeneo ya Vikindu, mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo na inadaiwa kuwa askari mmoja ameuawa kwenye mapigano hayo.
Chanzo: Mwananchi.

No comments:

Post a Comment