March 29, 2016

Hivi Ndivyo Umaarufu Unavyomtesa Mrembo Jini Kabula

post-feature-image
Tamthilia ya Jumba la Dhahabu ndiyo iliyomtambulisha Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ kwenye tasnia ya filamu kutokana na uigizaji wake mzuri.

Jina la Jini Kabula lilitokana na kuigiza kama joka kubwa,uwezo mkubwa alioutumia katika kuigiza tamthilia hiyo iliwafanya watu wengi waamini kwamba yeye ni jini kweli.

Katika hali ya kusikitisha, Jini Kabula alionekana hakuridhika na umaarufu huo kwani baada ya tamthilia hiyo kupotea machoni mwa Watanzania alianza kujiingiza kwenye ulevi, kuvaa nusu uchi na madai ya kutoka kimahaba na baadhi ya wasanii wenzake wa kike.

Hata hivyo kwa sasa msanii huyo amekuwa kimya tofauti na miaka ya nyuma ambapo alikuwa hakosekani kwenye magazeti mbalimbali nchini. Kitendo hicho kilisababisha paparazi wetu kufunga safari ya kumtafuta kwa lengo la kutaka kujua ukimya huo una heri?

Fuatilia…

Swagazz: Mbona upo kimya sana, hata kwenye magazeti hatuoni tena ukiandikwa kama zamani?

Jini Kabula: Kila jambo lina wakati wake, nimempata mwanaume ambaye hataki mambo ya kijinga. Kwa kiasi fulani ni kama ufahamu wangu umefunguka na sasa najuta kuwa maarufu, natamani kurejea hali yangu ya kawaida lakini nashindwa.

Swagazz: Hee! Baadhi ya wasanii chipukizi wanasaka umaarufu kwa gharama kubwa ikiwemo ya kutengeneza skendo ili waandikwe kwenye vyombo vya habari na kurushwa kwenye mitandano ya kijamii, kulikoni?

Jini Kabula: Najuta kwa sababu kuna baadhi ya skendo huwa zinaandikwa bila mimi kuzifanya hali ambayo huwa inasababisha nyumbani na jamii kwa ujumla inichukie kutokana na matendo hayo.

Swagazz: Kuigiza kama jini kumeathiri vipi maisha yako?

Jini Kabula: Nimeathirika kwa sehemu kubwa sana. Wapo baadhi ya watu mpaka sasa wanajua mimi ni jini kweli kutokana na urefu wangu, kuna baadhi ya nyumba nyingine nikifika huwa wananikimbia huku watoto wakipoteza fahamu kwa kuniogopa.

Kwa kweli hali hiyo inaniumiza sana japo wakati mwingine huwa nacheka tu kwa kujua ujumbe nilioukusudia umeifikia jamii. Na hii ndiyo sababu nasema nauchukia umaarufu kwa sababu wakati mwingine nakosa uhuru wa kutembea kama watu wengine wasiojulikana zaidi kwenye jamii.

No comments:

Post a Comment