Mwanamume
aliyeteka nyara ndege ya shirika la Misri la EgyptAir na kuishurutisha
kutua Cyprus amekamatwa, wizara ya mashauri ya kigeni ya Cyprus
imetangaza.
Mwanamume huyo alidai kwamba alikuwa na mkanda wa kujilipua na kumwamuru rubani wa ndege hiyo kuielekeza Cyprus au Uturuki.
Ndege hiyo, iliyokuwa safarini kutoka Alexandria hadi mjini Cairo, mwishowe ilitua uwanja wa Larnaca nchini Cyprus.
Abiria karibu wote walikuwa wamefanikiwa kuondoka kutoka kwenye ndege hiyo.
Ripoti
zinasema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir anataka kuongea na mkewe
walietengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea
katika uwanja huo wa ndege.
EgyptAir: Mtekaji ataka kumuona ''mkewe''
Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi.
Akijibu
maswali ya waandishi iwapo mtekaji huyo alishinikizwa na mapenzi,
alicheka na kusema, ''kila mara kuna mwanamke anayehusishwa''.
Shirika
la habari la Cyprus CYBC linasema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na
malengo yake ya kibinafsi, mtekaji huyo alikuwa na mkewe waliyetengana
nchini Cyprus.
Walioshuhudia
wanasema kuwa mtekaji huyo alirusha barua katika uwanja huo wa ndege
ilioandikwa Kiarabu akiomba ipelekwe kwa mwanamke huyo.
No comments:
Post a Comment