Nimeoa mwaka 2009 na tumebahatika kuzaa watoto wawili.Kwa hivi sasa ndoa
yangu imeyumba zaidi kwani unyumba ninapewa kwa mwezi mara mbili tena
kama msaada.
Kuna dalili zote mke wangu amepoteza mvuto na mimi kwani hata nikihitaji
penzi amekuwa unwilling, lakini mke wangu ana mdogo wake wa kike ambaye
ni robo tatu mama mwenye nyumba kwasababu anafanya kila kitu nyumbani.
Mke wangu yeye akitoka kazini ni kusingizia amechoka basi nikuwasha Tv
kuangalia tamthilia ni takribani miezi miwili sasa, uhusiano wetu na
mdogo wake ulianza kuchukua sura mpya ile tabia ya kuniwekea chakula
mezani imehamia kuniletea chumbani cha ajabu leo asubuhi kaja kunidekia
chumbani na night dress dada yake akiwa kazini.
Moyo wangu kama binadamu umeanza kumuangukia na alichonieleza dakika
ishirini zilizopita ni kwamba dada leo atalala msibani nyumba ya pili
kwa hiyo atakuja kulala kwangu nimepigwa na butwaa.
NAOMBENI USHAULI NIMKEMEE PEPO AU NIFUTWE MACHOZI
No comments:
Post a Comment