March 22, 2018

EMANUEL MBASHA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU KUTOKA NA AGNES MMASY

Msanii wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha amefunguka na kuamua kuweka wazi mahusiano yake na mwanamitindo maarufu nchini agnes mmasy na kusema kuwa watu wamekuwa wakizusha kuhusu yeye kutoka kimapenzi na mwanadada huyo lakini taarifa hizo sio za kweli.

Katika Ukurasa wake wa instagram , Mbasha aliandika “Nakanusha yote ni uongo, sia mahusiano na huyu dada kabisa na wanaoendelea kuzusha  na kueneza huu uongo basi na mungu wangu atawalipa.sio kweli.”

Kumekuwa na tetesi katika mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano kati ya mwimbaji huyo na mwanadada huyo ambaye ni mwanamitindo ambaye amekuwa akipiga picha za uchi mara nyingi na kuziweka katika mitandao ya kijamii

Hata hivyo kwa rekodi ya hivi karibuni, Emmanuel Mbasha alikiri kutokuwa na mwanamke tangu alipoachana na mke wake Florah na kusema kuwa kwa sasa  amejikita zaidi katika swala la uokovu na kwamba kuwa na mahusiano kabla ya ndoa ni kuzini na asingependa kufanya kitu hicho.


No comments:

Post a Comment