HAYA ni mazito! Nyuma ya shughuli ya kuolewa kwa staa wa sinema za
Kibongo, Wastara Juma na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma
iliyofungwa Alhamisi iliyopita, kuna matukio ya kustaajabisha ambayo
Ijumaa Wikienda limeyabaini.
Ndoa hiyo iliyofungwa kimyakimya, ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita
nyumbani kwa mwigizaji huyo, Tabata-Barakuda, jijini Dar ambapo
ilihudhuriwa na watu wachache tofauti na ilivyotarajiwa kutokana na
umaarufu wa wanandoa hao.
NDOA ILIFUNGWA KWA SIMU
Imebainika kuwa, awali ndoa hiyo ilikuwa ifungwe saa kumi jioni na
baadaye kuelezwa ilisogezwa mbele hadi saa 12 jioni, hata hivyo
haikufungwa muda huo baada ya bibi harusi kuchelewa kufika akitokea
saluni alikoenda kupambwa na kulazimika shehe afungishe ndoa hiyo kwenye
simu wakati Wastara akiwa kwenye foleni barabarani.
BWANA HARUSI AGOMA KUPIGWA PICHA
Imeelezwa kuwa, baada ya bwana harusi kutinga na wapambe wake alitoa
onyo kali huku likisisitizwa na wapambe wake kuwa hairuhusiwi kupiga
picha na kutuma kwenye mtandao wowote wa kijamii kwa vile ndoa hiyo
ilikuwa ya siri.
AGOMA KUMFUNUA BIBI HARUSI
Katika hali ya kushangaza, baada ya bibi harusi kuwasili aliingizwa
katika chumba maalum kwa ajili ya kumsubiri mumewe na hata alipoingia
ndani, shehe alimuomba amfunue mkewe ili kumhakikisha kama ndiye yeye
kitu ambacho alikipinga na kudai hakuwa na shaka naye na kuomba
waendelee na kitu kingine.
WASTARA ASHINDWA KUPATA MSOSI
Jambo lingine ambalo lilizua minong’ono ni Wastara kushindwa kupata muda
wa kula chakula ambacho kiliandaliwa kwa sababu baada ya kumaliza
kupiga picha za familia na kushikana mkono na mumewe, mumewe alimtaka
waondoke huku akimwambia dereva wao awashe gari.
WADOGO WA SAJUKI WALIA
Katika hali ambayo haikuweza kufahamika mara moja, wadogo wa aliyekuwa
mumewe wa pili wa Wastara, merehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Mohamed
Kilowoko na Njegere Kilowoko waliangulia kilio kwa kile walichodai
walikuwa na huzuni na furaha.
January 12, 2016
Mazito Yaibuka Ndoa Mpya ya Wastara...Ndugu wa Marehemu Sajuki Waangua Kilio
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment