Nimekuja kwenu nahitaji ushauri, ni urgent.
Hapo katikati niligundua kuwa Mr wangu ana kimada, tukasumbuana na
kugombana sana juu ya hilo, ingawa sikumshika live ila ni wazi kwamba
alikua nae, mbali na hilo pia ni mlevi kupindukia.
Nilipoona suala hilo linaendelea nikaona isiwe tabu, nikatafuta suluhisho.
Na mimi nikatafuta mtu pembeni aniliwaze, kuna dereva tax huwa tunamtumia sana kwa shughuli za kifamilia,
Nikaamua kumzawadia penzi huyo jamaa, sio kwamba nilimuanza mimi, bali alikua akinisumbua siku nyingi, hivyo nikaona nimkubali.
Katika mara zote nilizokutana nae (6) niligundua kwamba hajiwezi kabisa,
nikaona this relationship is not worth it, nikampiga chini, pia mtu
mwenyewe hana hata Chumba cha kulala, Mara zote anaazima Chumba kwa
mwenzie, ingawa ukimuona kwa nje ubrazamen alionao huwezi amini, ni type
ya wale wanaume wenye kuongea sana na mbwembwe nyingi lakini hamna
lolote.
Nikakata mawasiliano nae na kumwambia asinitafute tena, akaanza
kunililia nisimwache, anapiga simu muda wote kunibembeleza, kila
akiniona hata na watu wengine Mtaani, labda Dukani n.k atakimbia haraka
kuja na kuomba tuongee pembeni hadi kero.
Hivi karibuni nimepata mtu mwingine mahali nakoabudu, he is so caring,
ni mtu mwenye Upendo sana, hanywi pombe na ananipenda kwa dhati, he is
god fearing and above all his performance is much better than my husband
and the tax driver's.
Juzi kumetokea shida kubwa baada ya Mr kushika sms ya yule tax driver
akiendelea kunibembeleza, Nikalazimika kusema kuwa jamaa ndio
ananifuatilia, ananitaka kimapenzi, akasema kama ni kweli na ili
aniamini Basi tufanye fumanizi la kutengeneza, kwamba nikubaliane na
yule kijana wa tax kwenda nae guest na yeye aje atufumanie na kundi la
mabaunsa wamwoe wote.
Nikikataa mpango huo basi atajua nilishatembea nae, na mimi najua yule
tax driver kwa vyovyote vile atauvaa huo mtego, namuonea huruma sitaki
apate aibu hiyo wakati tulishaachana nae.

No comments:
Post a Comment