Mmoja wa ndugu wa marehemu akifarijiwa.
Polisi katika Jimbo la California nchini
Marekani wametaja majina ya washukiwa wawili ambao wameuawa kwa
kuhusika na vifo vya watu 14 waliouawa kwa kupigwa risasi katika Mji wa
San Bernadino jana.
Watu hao ambao ni mwanaume na mwanamke
waitwao Syed Rizwan Farook, 28, na Tashfeen Malik, 27, wameuawa kwenye
ufyatulianaji wa risasi na polisi.
Farook alikuwa ameajiriwa na baraza la mji kwa miaka mitano, mkuu wa polisi wa San Bernadino Jarrod Burguan ameeleza.
Shambulio hilo lilitokea jana wakati wa hafla katika ofisi moja. Maelezo kuhusu waliofariki bado hayajatolewa.
Tukio hilo ni baya zaidi katika matukio
ya ufyatuaji wa risasi dhidi ya umma nchini Marekani tangu watu 26
wauawe katika shule moja mjini Newtown, Connecticut mwaka 2012.
Ramani inayoonyesha tukio lilipotokea.
Bw. Burguan, amesema watu 17
walijeruhiwa na kwamba polisi wana kila sababu ya kuamini kwamba wawili
hao pekee ndio waliohusika kwenye shambulio hilo.
Shambulio lilo lilitekelezwa katika
kituo cha Inland Regional Center ambacho huwasaidia walemavu na watu
wenye matatizo ya kiakili. Hata hivyo, ufyatuaji risasi huo hauonekani
kuwa na uhusiano na wagonjwa hao.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache tu baada ya watu watatu kuuawa katika kliniki ya Colorado Planned Parenthood.
Rais wa Marekani, Barack Obama ameshutumu shambulio hilo.
“Jambo moja tunalojua ni kwamba visa hivi vya ufyatuaji wa risasi humu nchini haviwezi kulinganishwa na kwingine duniani.”
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Kijasusi la FBI David Bowdich anasema sababu kubwa ya mauaji hadi sasa haijafahamika.
“Kwa wakati huu ninaelewa moja ya
maswali yenu ni kuhusu tukio hili la kigaidi. Ninawaeleza sasa kuwa
hatujui kama hili ni tukio la kigaidi kwa hiyo tunaanzia mwanzo kufanya
kazi na wenzetu waliopo katika eneo hili.
Credit: BBC
No comments:
Post a Comment