Kubenea |
Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Massaburi, amefungua kesi ya kupinga ushindi wa Saed Kubenea, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Dk. Massaburi amefungua kesi hiyo ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Mbali
ya Kubenea, wengine waliounganishwa katika kesi hiyo ni Masimamizi wa
Uchaguzi katika jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika
kesi hiyo, Dk. Massaburi anadai kwamba mshtakiwa wa kwanza (Kubenea),
alitoa rushwa ya kununua jenereta katika hospitali ya Mavurunza iliyopo
kata ya Kimara, kutoa rushwa ya ujenzi wa barabara ya Matete, kutoa
zawadi kwa kununulia ‘Pool Table’, kwa ajili ya kuwashawishi wananchi
wampigie kura.
Madai
dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo ni hakumpatia nafasi ya
kuhesabu kura upya kama alivyoomba, hakumjulisha tarehe, muda na wapi
matokeo ya jimbo hilo yalikuwa yanajumulishwa, yeye na mawakala wake
hawakuona wakati vifaa vya uchaguzi vinafunguliwa.
Pia
anadai kwamba baadhi ya vituo havikufanya uchaguzi, na pia baadhi ya
wapigakura walipiga kura wakati hawajafikisha umri wa kupiga kura.
Katika madai hayo, Dk. Massaburi anaiomba Mahakama Kuu itengue ushindi wa Kubenea uliotangazwa na Msimamzi wa Jimbo hilo.
Akizungumza na mtandao huu
jijini Dar es Salaam jana, Kubenea alithibitisha kupokea madai hayo
kutoka kwa Dk. Massaburi na kwamba ameombwa kuwasilisha utetezi wake
katika mahakama hiyo ndani ya siku 21.
Aidha,
Kubenea alisema katika kesi hiyo, atawakilishwa na jopo la mawakili
watano akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, Mabere Marando,
Peter Kibatala, Method Kimongoro na Frederick Kihwelo na kwamba
wamepanga kuwasilisha utetezi wao ndani ya wiki hii.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment