Jambo limezua jambo! Kufuatia tumbuatumbua inayoendeshwa na Rais Dk.
John Pombe Magufuli kwa vigogo waliokuwa wanawapa jeuri mastaa wa kike
mjini, wenyewe wameibuka na kusema kiongozi huyo ‘amewaua’ kwa njaa.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa mastaa wengi wa kike
wanalalamika njaa na ndiyo maana tangu alipoingia madarakani Rais
Magufuli na kuanza kuwaondoa mafisadi, wasanii hao wamekuwa hawaonekani
viwanja kama zamani kwa sababu hawana mkwanja.
“Yaani wasanii wa kike wana hali mbaya sana ndiyo maana hamuoni
wakiwa na mbwembwe kama zamani wamekuwa wakijifungia ndani tu hawataki
kuonana na watu kwani hata hela za kwenda saluni kujiremba hamna maana
wanasema waliokuwa wakiwapa jeuri wengi wao wamekumbwa na tumbua majipu,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata ubuyu huo, paparazi wetu aliwatafuta baadhi ya mastaa ambapo walikuwa na haya ya kusema;
ISABELA MPANDA
“Kweli tumeathirika sana na hii tumbua majipu maana waliokuwa
wakitupa fedha nyingi hata ukiomba milioni wanatoa kwa sasa wanaogopa
hata ukiwapigia simu hawapokei huku wengine wakiwa ni wale vigogo
waliokamatwa, Rais Magufuli ametunyoosha.”
BABY MADAHA
“Kiukweli lazima iathiri kwa sababu ilikuwa rahisi kwa mtu kudhamini
hata katika muvi. Kipindi cha Kikwete (Jakaya, Rais wa awamu ya nne) mtu
anakupa milioni 20 au 30 kwenye muvi lakini sasa hivi, thubutu.”
MIRIAMU JOLWA ‘JINI KABULA’
“Mimi sina kawaida ya kutoka na mapedeshee, bwana’ngu ni wa kawaida sana kwa hiyo sijui kama imeathiri vipi hiyo tumbua majipu.”
Chanzo: Global Publishers
December 28, 2015
Home
/
Unlabelled
/
Mastaa wa Bongo Movies Walia na Tumbua Tumbua Majipu ya Rais Magufuli..Wadai Imewaletea Njaa.......
Mastaa wa Bongo Movies Walia na Tumbua Tumbua Majipu ya Rais Magufuli..Wadai Imewaletea Njaa.......
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment