KAMATI Maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar chini ya Mwenyekiti
wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein imewataka
wananchi na wanachama kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza katika
uchaguzi mkuu wa marudio.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride
Bakari Jabu, wananchi wametakiwa kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio na
kuachana na propaganda zinazotolewa na watu wachache kwa lengo la
kupotosha ukweli.
“Kikao cha Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar kilichokutana hapa chini ya
Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar, Dk Shein kimewataka wananchi,
wanachama na wafuasi wa CCM kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa marudio
ambao tarehe ya kufanyika kwake itatangazwa na taasisi husika,” imesema
taarifa hiyo ya Waride.
Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25 ulifutwa na Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kwa kile
alichoeleza ni kuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi huru
wa kidemokrasia.
Katika kikao cha jana kilichohudhuria pia na viongozi kadhaa wa kitaifa
akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan, kilijadili ajenda mbili ikiwemo hali ya kisiasa mara baada ya
uchaguzi mkuu kwa upande wa CCM.
Katika taarifa hiyo, chama hicho kimesema kimeridhishwa na mwenendo wa
hali ya kisiasa na kimewapongeza wanachama waliojitokeza kwa wingi
kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Aidha chama kimepongeza na kutoa baraka kwa mazungumzo yanayoendelea ya
viongozi wakuu wa kisiasa yakiwa na lengo la kuleta amani ya kudumu.
Kamati ya mazungumzo ya hali ya kisiasa Zanzibar yenye lengo la kusaka
amani ya kudumu iliyovurugika kutokana na kufutwa kwa uchaguzi mkuu
inaundwa na viongozi wastaafu wakiwemo marais, Dk Salmin Amour, Amani
Abeid Karume, Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad na Rais
wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Akizungumza juzi Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais wa Zanzibar, Dk Shein
alisema mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na taarifa kamili
yatakapofikia tamati. Alipoulizwa kuhusu hatma ya CCM kama uchaguzi mkuu
utarudiwa, Waride alisema chama bado kiko imara na hakijatetereka.
“Wapo wanaosema CCM imeyumba, si kweli wala CCM haijapoteza majimbo kwa sababu kura hazikumalizwa kuhesabiwa,” alisema.
December 28, 2015
Home
/
Unlabelled
/
CCM Yajipanga Kurudia Uchaguzi Zanzibar.......Yawataka Wanachama Wake Kujitokeza Kwa Wingi
CCM Yajipanga Kurudia Uchaguzi Zanzibar.......Yawataka Wanachama Wake Kujitokeza Kwa Wingi
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment