Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo.
IMEVUJA! STAA wa muziki na mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo
amedaiwa kuasi kanisani kisa kikitajwa ni kutokana na ujauzito alionao,
unaohusishwa na mkali wa Bongo Fleva, Abdul Saleh Kiba.
Chanzo makini cha gazeti hili ambacho kiko karibu na mwanadada huyo,
kilisema kwa muda sasa amekuwa haonekani kanisani kama awali, na hata
kwenye kwaya aliyokuwa akiimba ndani ya kanisa analosali la St. Peter
lililopo Oystebay jijini Dar, haonekani.
“Yaani Jokate ujauzito alionao unamsumbua sana, ameacha hata na kuimba
kwaya, kanisani haonekani kama ilivyokuwa zamani, pia hali hiyo
inachangiwa na kwamba anaona aibu amebeba mimba nje ya ndoa, yaani
hajaolewa ndiyo maana mara nyingi haendi kanisani,” kilisema chanzo
hicho.
Baada ya kupata habari hizo waandishi wetu walifunga safari mpaka
kanisani kwa ajili ya kuonana na kiongozi wa kwaya aliyejulikana kwa
jina moja la Catherine, ambapo walimkosa na kufanikiwa kuzungumza naye
kwa njia ya simu baada ya kupewa namba zake.
“Jokate kwa sasa haimbi kwaya, amesitisha lakini sijui sababu ni nini,”
alieleza kwa kifupi baada ya kuulizwa juu ya upatikanaji wa mrembo huyo
maarufu kama Kidoti.
Ili kuleta mzani wa habari, Jokate ambaye ni mwandani wa mwanamuziki wa
Bongo Fleva, Ali Kiba naye alitafutwa na kuelezwa habari hizo, ambapo
alikuwa na haya ya kusema;
“Ni kweli siimbi kwaya mwaka sasa, ila kanisani sijaacha kwenda na
siwezi kuacha kwenda na bado kazi za kanisa nyingine nafanya, sijaacha
kwa sababu ya mimba bali ratiba zangu tu zilikuwa ngumu.”
No comments:
Post a Comment