WAKATI Rais John Magufuli akiwa kwenye zoezi la kutumbua majipu kwenye
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
mshtuko mkubwa umetokea kufuatia kigogo mwenye wadhifa wa Artsan One
(TPA) jijini Dar, Elia Eliampenda Kimaro (51) kufariki dunia ghafla kwa
shinikizo la damu (presha) akiwa nyumbani kwake, Mikwambe, Kigamboni,
Dar.
Kimaro alifariki dunia Novemba 30, mwaka huu kwa uthibitisho wa daktari
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako marehemu alikimbizwa kwa
ajili ya matibabu.
Kifo cha Kimaro kimetokea wakati kukiwa na sintofahamu kubwa miongoni
mwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuhusiana na utolewaji wa makontena 349
kinyemela na kuisababishia serikali kukosa mapato ya kiasi cha shilingi
bilioni 80.
Taarifa kutoka ndani ya familia, marehemu alisumbuliwa na maradhi hayo
kwa muda mrefu. Lakini ghafla alfajiri ya Novemba 30, hali yake
ilibadilika na hivyo kukimbizwa Muhimbili ambako daktari alisema
alishafariki dunia.
Mwandishi aliweza kufika msibani ambapo aliwashuhudia wafanyakazi wengi
wa bandarini na TRA bandarini wakiwa hapo kwa ajili ya maandalizi ya
mazishi.
Baadhi ya wafanyakazi hao, walisikika wakidai, marehemu alikuwa miongoni
mwa vigogo waliokuwa wakichunguzwa kwa utolewaji wa makontena 349 siku
chache zilizopita.
“Pia nasikia baada ya waziri mkuu (Kassim Majaliwa) kutoa mwongozo siku
zile bandarini, watu wa usalama wa taifa walishamfuata hapa kwake mara
kadhaa na kumhoji.
"Lakini pia, kuna madai kwamba, miamala yake ya kibenki nayo
ilifuatiliwa na jamaa hao ambapo walikuta pesa nyingi,” alisikika
akisema mmoja wa wafanyakazi hao ambaye alipogundua kuna waandishi wa
habar alifunga kinywa.
Nao baadhi ya waendesha bodaboda wa eneo hilo, walionekana kushangazwa
sana kufuatia taarifa za kifo cha kigogo huyo, wakidai siku moja kabla,
walionana naye akiwa mzima wa afya.
Hata hivyo, walisema mara baada ya taarifa za kifo, walishangaa kuona
magari yake ya kifahari yakiondolewa kutoka nyumbani kwake hapo:
“Labda waliyapeleka mahali ili kupata nafasi ya kuweka maturubai ya
msiba. Si unajua majumba haya ya ghorofa, yana nafasi zaidi ya kwenda
juu kuliko upana,” alisema mmoja wa bodaboda hao.
Mwendesha bodaboda mmoja alisema: “Mzee wa bandari alikuwa mtu poa sana.
Hata madereva wa daladala zake wameumia. Unajua jamaa alikuwa na
mkwanja wa maana. Hii nyumba ya hapa ‘cha mtoto’, ana nyumba nyingine
Yombo (Dar), magari ndiyo usiseme. Yaani tumempoteza mtu muhimu sana.”
Marehemu Kimaro alizikwa Desemba 2, mwaka huu kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. Ameacha mke na watoto wanne.
Credit: Risasi Jumamosi/Gpl
December 5, 2015
Kigogo wa Bandari Afariki Kwa Presha...Undani wa Kifo chake Waelezwa Hapa
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment