December 5, 2015

Diamond Platnumz na Mama yake Wakaa Kikao Kizito..Kisa Zari

Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mama’ke mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ wamelazimika kukaa kikao kizito ili kupata muafaka wa mzazi mwenzake na staa huyo, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kurejea Bongo na kuishi katika nyumba moja na mkwewe huyo ambaye walipishana kauli hivi karibuni.


Hivi karibuni, Zari aliyekuwa akiishi na mama Diamond nyumbani kwake, Tegeta-Madale jijini Dar, walipishana kauli na mzazi huyo sambamba na ndugu zake hadi kufikia hatua mrembo huyo aliyezaa mtoto mmoja na Diamond (Tiffah) kurejea nyumbani kwake Afrika Kusini kupisha kile alichokiita ni ‘uswahili’.

Chanzo makini kimeeleza kuwa, baada ya kuona Diamond anampenda Zari na mapenzi yao ni motomoto, familia haikuwa na jinsi zaidi ya kukaa kikao kulijadili kwa kirefu suala hilo na kupata muafaka ambapo habari njema ni kwamba, mama Tiffah anatarajia kutua Bongo siku chache zijazo.
“Diamond si unajua ndiyo kichwa katika familia. Amewaita ndugu akawaeleza dhamira na mikakati yake na Zari hivyo wamekubaliana arejee Bongo,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo, hakutaka kufunguka kwa undani akidai ni mambo ya kifamilia.

“Kila kitu kipo sawa. Zari ataibuka na maisha yataendelea kama kawaida, haya mambo ya kifamilia bwana,” alisema Diamond.

Kabla ya kufikia muafaka huo, Zari aliripotiwa kuwa anakuja nchini Desemba 8, mwaka huu wakati mama Diamond akionekana kupinga lakini hatimaye muafaka umepatikana.

GPL

No comments:

Post a Comment