Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ameishangaa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kutogawa bure Mashine za EFDs, na
wao kubaki na kazi ya kukusanya mapato.
Akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji jana jijini
Dar es Salaam, ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na Baraza
la Biashara la Taifa (TNBC), alisema muda uliopotea na kodi ambayo
haikukusanywa wakati wa mvutano na wafanyabiashara ungetosha kununua
mashine mpya na kuwagawia.
“Kama mnajua mashine hizi ni halali na ni zenu, wapeni bure kazi yenu
iwe ni kukusanya kodi, ni hesabu rahisi sana isiyohitaji kwenda chuo
kikuu kuwa muda uliopotea na fedha hazifiki bilioni 12 zingetosha
kununua na iwe kazi ni kukusanya kodi,” alisema.
Awali katika salamu zake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara,
Jonson Minja, alimpongeza rais kwa kazi kubwa aliyofanya Bandarini na
TRA kwa kuwa imewezesha kodi kukusanywa kwa usahihi na kwamba kipindi
cha nyuma fedha nyingi zilipotea, kutokana na mfumo wa ukusanyaji kodi
kutowekwa wazi.
Aidha, alisema mashine za EFDs zitatumika kwa wafanyabiashara wote
mwakani, kwa kuwa changamoto zilizosababisha mvutano baina yao na
serikali zimemalizika.
Aidha, alimtaka rais kufuatilia kwa karibu ukwepaji kodi katika sekta
isiyo rasmi na kwamba kukiwa na mipango madhubuti serikali itaweza
kupata kodi kwa wananchi wote.
“Kasi ya rais inatupa matumaini makubwa sana, tunachoweza kusema, Mungu
akubariki akupe hekima na nguvu...tunaomba uimarishe viwanda vya kati na
vidogo ili malighafi zisisafirishwe kwenda nje, bidhaa ambazo
zitasaidia kukuza uchumi na kuimarisha shilingi dhidi ya Dola ya
Marekani,” alisema.
Tangu mwaka juzi kulikuwa na mvutano mkali baina ya wafanyabiashara na
TRA, ambao waligoma kutumia mashine hizo hadi serikali
itakaposhughulikia kero zao ikiwamo bei ya mashine, utitiri wa kodi,
ukwepaji kodi na urasimu uliopo.
Wafanyabiashara kwa umoja wao waliitisha mgomo nchi nzima na kumekuwa na
mazungumzo ya mara kwa mara na serikali, ambayo wakati mwingine
hayakufikia ukingoni, hatua iliyofanya baadhi ya viongozi wa
wafanyabiashra kukamatwa.
Minja alikamatwa na Polisi mkoani Dodoma mwaka jana, na kuswekwa ndani,
jambo lililofanya wafanyabiashara kuitisha mgomo wa siku tatu hadi
serikali itakapoeleza alipo kiongozi wao.
Baadaye ilibainika anashikiliwa na Polisi mkoani humo, na alipandishwa
mahakama ya mkoa na kusomewa mashtaka ya kuchochea mgomo wa
wafanyabiashara nchini.
Baadaye mahakama ya mkoa ilimuachia huru kiongozi huyo.
December 5, 2015
Magufuli Aitaka TRA Kutoa Mashine za EFDs Bure.
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment