Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Jumanne Sagini ametoa siku 14 kwa
Afisa Ardhi, Mhandisi wa Majengo na Afisa Mipango Miji Manispaa ya
Morogoro kuandika maelezo ya kwanini wasifukuzwe kazi kutokana na
kufanya kazi chini ya kiwango na kukiuka maadili ya utumishi wa umma
Agizo
hilo limekuja kufuatia watendaji hao wa serikali kutumia vibaya mamlaka
waliyopewa na serikali ikiwemo kuruhusu ujenzi wa hoteli ya Flomi
iliyopo eneo la Msamvu mjini Morogoro, kujengwa katika eneo ambalo
wanajua limepita bomba la mafuta la TAZAMA.
Pia
kushindwa kuzuia ujenzi wa holela katika maeneo yasiyo rasmi pamoja na
kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya ofisi hizo.
Chanzo -GPL
No comments:
Post a Comment