October 6, 2015

Magufuli Abomoa Ngome Za Chadema Hanang, Mbulu Na Karatu.



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwaambia wananchi wa Karatu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani,kuwa mmoja wa viongozi wa upinzani anayempenda kwa dhati, ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Wilbrod Slaa
Mgombea Ubunge jimbo la Karatu Dk.Wilbald Slaa Lorri akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na yeye mbele ya wakazi wa mji wa Karatu jana jioni kwenye mkutano wa kampeni,kulia kwake ni  Wabunge watarajiwa viti maalum wanaowakilisha wanawake mkoa wa Arusha, kushoto ni Catherine Magige na Violet Mfuko wakishangilia.  
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli pichani kushoto akiungana na wasanii Chege na Temba kucheza muziki wakati wa  mkutano wa kampeni  mjini Karatu, mkoani Arusha.

Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Mbulu, mkoani Manyara jana  jioni
 Dkt. Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi wa Mbulu jana jioni  kwenye mkutano wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwanadi wagombea ubunge na madiwani mbele ya wakazi wa mji wa Mbulu kwenye mkutano wa kampeni jana jioni
Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment