May 6, 2015

UMESIKIA STORI KUHUSU NEY NA DIAMOND KUWATUNGIA NYIMBO EX GIRLFRIEND ZAO IPO HAPAAAA CHECK OUT



Diamond na Nay wa Mitego wakiimba ngoma yao ya Muziki Gani.

Na Musa Mateja
DONGO! Wakali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ wameamua kuwavua nguo waliokuwa wapenzi wao kwa kuandaa wimbo ambao unazungumzia matendo machafu waliyowahi kutendewa na wapenzi wao hao.

Mashabiki wakijiachia.

Ngoma hiyo inayofahamika kama Mapenzi Pesa ambayo inaachiwa leo katika vituo mbalimbali vya redio, mastaa hao wameimba kwa staili ya kubishana kwa kuambiana kuwa mapenzi ni pesa mwingine akisema si pesa ila ni kupetipeti.

Akizungumza na Risasi Vibes, mmoja wa watu wa karibu na wasanii hao alisema kwamba, Diamond na Nay wa Mitego, wameamua kuvunja ukimya kupitia wimbo huo ambapo wamezungumza mambo yote waliyowahi kutendewa na wapenzi wao ikiwa kama njia ya kutoa kilio chao kwa jamii ambayo ilikuwa ikiwaona wao kama ndiyo wakosaji baada ya kutofautiana nao.

“Wameurekodi makusudi kabisa kufikisha ujumbe kwa mashabiki wao hasa ambao wengi hawakuweza kujua visa vya wasanii hao kuachana na wapenzi wao na kikubwa zaidi ni kuonesha kuwa mtu hata kama una pesa kiasi gani au unaonesha upendo wa aina gani lakini kama mwanamke akiamua kufanya yake, anafanya tu,” alisema mtu huyo wa karibu.


Risasi Vibes baada ya kunasa ishu hiyo, iliwasaka Diamond na Nay ili waweze kuzungumzia wimbo huo na kueleza ni kipi kilichowafanya hadi wakaamua kuingia studio na kuimba mambo ambayo kila mmoja yamemtokea kutoka kwa mpenzi wake. Majibu yao yalikuwa hivi:

“Kiukweli niliguswa sana baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wangu Siwema hasa kutokana na namna tulivyoachana, hapo ndiyo nilijua kuna baadhi ya wanawake hata uishi naye kwa mapenzi yapi na umpatie pesa kiasi gani bado suala la kutulia linategemeana na yeye tu anavyochukulia,” alisema Nay.

“Naweza kusema kuwa watu wanatakiwa kuelewa kuwa sisi ni wasanii hivyo kuna muda inatakiwa kabla hujaimba jambo kuhusu wengine basi kuna muda mzuri pia ambao tunatakiwa kuimba kuhusiana na mambo ambayo sisi wenyewe tumefanyiwa ili kuwafahamisha mashabiki wetu, najua kupitia wimbo huu kuna watakao tuelewa na wengine wataona kama tumeongea mambo ya chumbani sana lakini ukweli utabaki tu kuwa sanaa ina namna nyingi ya kufikisha ujumbe kwa mashabiki, hivyo naomba mashabiki wakae makao wa kula Jumatano (leo) watapata kila jambo ndani ya wimbo wetu huo,” Diamond.

No comments:

Post a Comment