Alinitumia friend request FB .. Baada ya kumkubalia urafiki sikujua yeye ni nani na anafanya nini na hii ni kawaida yangu mtu ambae huwa nina mfahamu au tumekua marafiki kwa muda mrefu ndio naongiaga kwenye profile zao... Tuli chat Mara kadhaa nikiwa najua tu kijana tu Kama vijana wengine.... Baadae alichukua number yangu yangu kupitia page yangu FB ... Mara kazaa alikua ananipigia usiku mida ya saa tano saa sita akiwa anaomba tuonane: hallo
Hallo
Naweza kukuona ?
Mm nilikua nashangaa sana inakuaje gafla halafu si ki heshima as nikwamba mtu ana kununua
Nikamjibu unapigiaje cm gafla unataka kuniona usiku ?
Ananinijibu ndio nimeingia
Namuuliza kwa nn usinipe taarifa kabla ya siku kazaa Kama unataka kuniona ? Mm siwezi na huwezi kunikurupua kiasi hicho! Kumbe yeye alikua anatumia umaarufu wake na uongozi wake wkt huo mm sijui yeye ni nani
Akaendeleaga kunipigia usiku gafla Kama kawaida yake na mm sikuwahi kwenda , halafu nilikuaga hata number sija isave kutokana na namna anavyo ongea. kila akinipigia namuuliza wewe nani ?
Anani jibu mm fulani (jina lake sipendi kuliweka hapa ) kwa yeye akawa anazani namjua ! sasa nikamuuliza cousin wangu Farida hivi unamjua huyu mtu anaitwa mtu fulani
A kasema ndio .... Ndio nikaamua Sasa kuingia kwenye profile yake nikaangalia picha zake ... Ndio nikamjua na Farida akamiambia napenda sana huyo nyimbo zake nzuri sana marehemu dada yetu pia alikua anampenda! Kiukweli mm sikua najua nyimbo zake Lkn kuna nyimbo yake moja nilikua na jiua ila sikua na jua Kama ni yeye ndio kaimba.. Farida akawa ananiambia nyimbo zake basi tukawa tuna tabasamu .. Tukajiona tuna bahati kumjua Lkn Sasa tatizo lilikua ni namna alivyo kuwa ana niita ndio sikupenda na baada ya kumjua pia nilitamani kumuona live Lkn nilijikaza sana kwa sababu sikupenda ambavyo ! Alikua ananiita gafla usiku halafu pia maongezi yake kwenye cm hayakua ya kawaida sana kwa hiyo ni Kama mtu Fulani anae tumia jina lake na mm nika kaza kwa hiyo sikuwahi kwenda kabisa ....basi nilimpotezaa sana kwa muda mrefu ! Kuna siku tukakutana online akawa ana nitongoza rasmi ! Hapo sasa tayari nilikua nimesha mjua kuw yeye ni msanii , nikawa namwambia bwana mm naomba tuwe marafiki tu wa kawaida
Akanijubu mwanamke mzuri Kama wewe huwezi kuwa Rafiki yangu tu mm siwezi
Nikamwambia mm na mpenzi wangu na hapa nilipo na Pete ni mchumba wa mtu
A kasema ndio hivyo Kama hutaki kutoka na mm basi Lkn wewe kuwa Rafiki yangu siwezi
Mmh nikashangaa maana yeye alikua ni msanii wa pili kuniambia hayo maneno msanii wa mziki kuwa hawataki urafiki ( shabiki wao ) kuna time niliona Kama ana nyima haki ya kuwa shabiki wake nikamtole mfano wa huyo msanii mwingine nikamuuliza kwani nyie mkoje mpaka mlale na mtu ndio mjione wanaume ? Basi tukaishia hapo kuchat akiwa Anaendelea kusisitiza ana taka kuni... Tena anataja lile neno gumu ! Alinistaajabisaha yaani nili zoea kutongozwa kistaarabu kwa heshima Lkn hapo heshima ilikua 0. Baada ya kukataa kumuona kwa muda akaanza kuniambia unaogopa kuniona kwa sababu wewe sio wa kwenye hizo picha ninazo ziona FB Kama kweli ni wewe unge niona ... hahahaa nikacheka sana nikagundua kuwa kumbe kuna watu wanao wekaga picha ambazo sio zao tukawa tunaanza kubishana mm na mwambia ni mm yeye anasema si mm .... Na mm ktk uhalisia ni mbishi na ubishi wangu natakaga mpaka ukweli ueleweke ... Nikahisi Kama ametumia njia hiyo ili anione Lkn na mm nikawa najiuliza kwa nn anione mm muongo ? Wkt sio ? Lkn bado sikwenda kumuona kwa ajili ya hilo! Sasa ikafika siku naenda Dodoma kumuona baba yangu alikua mgonjwa ( mm nimzaliwa wa Dodoma na ndio kwetu kwa wazazi wangu , nimesoma na kukua huko ) nikiwa njiani nikamfikiria maana kwa wakati huo yeye alikua Dodoma kikazi...nikampigia nikamwambia Niko njiani naenda Dodoma ...
Akanijibu akamiambia dah na mm Niko njiani naenda hivi kuna vurugu zimetokea inabidi nikazitulize Lkn kwa jinsi ninavyo tamani kukuona kesho hiyo hiyo nageuza hata nikifika usiku ntakushtua
Nikamjibu poa
Kiukweli Dodoma mm huwa nikienda napenda sana disco kwa sababu huwa nakutana na marafiki zangu tulio soma wote na watu ninao wafahamu Sasa na yeye kwa sababu ni msanii nikaona Kama tukitoka wote itakua mizuka ... Basi kweli kesho yake akageuza akanipigia Niko sehemu flani ...nikamwambia poa mm leo naenda club anasema basi njoo nichukue nikamwambia poa... Nikawasha gari mpaka alipo nikapiga cm haijapokelewa ! Nikaona mmh sijui ndio tabia za kisanii ? Samahani kwa kusema hili mm naonaga wasanii wengi WASHAMBA ! Nimesema washamba kwa sababu kwanza hawajui ku keep ahadi na wanaonga kwa ajili ya jina tu wao ni kila kitu ....Ni kasema Sasa haya mambo gani basi nikageuza gari nikaenda zangu club ....nikiwa njiani akanipigia uko wapi ?
Niko njiani naenda club nimekuja mpaka hapo huku pokea cm nikaamua niondoke , akasema njoo nikamwambia siwezi kurudi Kama ukitaka kuja njoo wewe mm siji tena ... Basi akasema poa ... Niko club Mara nikamuona na marafiki zake Sasa nikawa naona Noma kwenda nikawa namtizama kwa mbali japo nilikua karibu nae.... kiukweli hata mm nilikua nimeanza kutamani kumuona kwa karibu.... Itaendelea
No comments:
Post a Comment