September 11, 2015

Mwigizaji wa Filamu Diana Kimari Akiri Kuanza Mapenzi ‘Utotoni'

CONFESSION! Msanii wa filamu Bongo, Diana Kimari ameanika ukweli wa moyoni kuwa, alianza kujihusisha na mambo ya mapenzi akiwa anasoma shule ya msingi.

Akipiga stori na Amani, Diana alisema alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi akiwa darasa la saba na hii ni baada ya kuingia kwenye utu uzima ‘kuvunja ungo’ kitu ambacho huona kwamba zile zilikuwa akili za kitoto na kwamba hakukuwa na ‘ladha ya mapenzi’ hivyo huwa hataki kukumbuka kabisa nyakati hizo.



“Ni kweli mimi si mgeni wa mapenzi, niliwahi kuwa na mpenzi tangu nikiwa shule ya msingi, japo hayakuwa na ladha maana si unajua mapenzi ya utotoni tena? Kwa sasa sina tena hamu na wanaume, nimeshaumizwa sana na mapenzi, sasa mimi na shule tu,” alisema Diana anayesomea biashara katika chuo kimoja kilichoko mkoani Kilimanjaro.

Chanzo: GPL

No comments:

Post a Comment