KATIKA hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata shughuli pevu kumkamata staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye alidaiwa kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali, Amani linakupa mchapo.
Timu iliyofika nyumbani kwa Wema Sepetu kumkamta kwa usumbufu aliosababisha kwa majirani.
Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo, Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake aliyejulikana kwa jina moja la Neema.
Awali, mapaparazi wetu walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema ambaye alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake na kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero.
“Kwa kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga muziki mkubwa katika sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana (usiku wa Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzia saa mbili usiku mpaka asubuhi na majirani walimfuata Wema mara kadhaa kumtaka apunguze sauti lakini aliwajibu vibaya.
Polisi akisimamia zoezi hilo kwa kuwawajibisha wahusika (mmiliki wa muziki na mwenye sherehe).
“Njooni mshuhudie wenyewe, tumeita polisi wamkamate,” alisema jirani mmoja.
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.
Mwenye sherehe, Neema( rafiki wa Wema Sepetu) akichukuliwa kwenye bajaji.
“Kwa sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina lake halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao katika ofisi za mtendaji, Kijitonyama kwa ajili ya hatua za kisheria,” alisema.
Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumza na gazeti hili, mwenyekiti wa mtaa huo, Mzee Haogwa, alithibitisha kuletewa malalamiko ya Wema na kufika nyumbani hapo ambapo pia alidai alishangazwa na kitendo cha kuwakuta wanaume tata kwenye sherehe hiyo.
No comments:
Post a Comment