Hapa akiwa na wanafunzi wenzake wanacheza mpira
kikongwe yuko mazoezini
Yuko darasani makini sana akimsikiliza
mwalimu wake
Mwalimu akimwelekeza kuandika
Yuko na wanafunzi wenzake darasani
Yuko shambani siku za mapumziko
Huyu ni Mariam Ong'ang'o Oloo mwanafunzi mpya katika shule ya msingi Obambo huko nchini kenya,sio kwamba ni mwanafunzi mkubwa kuliko wote darasani kwake,bali pia ndo mzee kuliko wote katika shule hiyo.Ana mika 78 lakini ndo kwanza ameanza darasa la kwanza.
Ololo ambaye anatokea Siaya huko nchini Kenya,
alianza shule rasmi tar 14 may mwaka huu akiwa ndani ya sare za shule huku nywele zake akiwa amezikata vizuri na alisindikizwa na mtoto wake wa kwanza George mwenye umri wa miaka 56.
Mwalimu mkuu Joseph Muloand alisema haya ni maajabu na lazima wawe na kazi ya ziada ya kumfundsha.
Hata hivyo Ololo mwenye watoto 8 amekuwa akikosa kuwa darasani kutokana na udhaifu wa mwili wake.
KWA NINI OLOLO ALIAMUA KWENDA SHULE WAKATI NI MZEE SANA.
Anasema kilichomvutia zaidi ni mambo ya Siasa na uchaguzi mkuu uliofanyanyika hivi karibuni nchini kwake.
Anasema Uhuru Kinyata sio mzee na amekuwa Rais wa 4 wa Kenya kwa sababu tu ya Elimu,hivyo basi mtu hawazi kuwa juu katika jamii kama hana elimu.Hayo ni mawazo ya bibi kizee Mariam Oloo.
No comments:
Post a Comment