WANAFUNZI wawili wa darasa la pili wenye miaka tisa na nane wa shule ya Msingi Kikunku wameshikwa na walimu wao kutokana na tabia yao ya kufanya mapenzi katika umri mdogo na kusababisha walimu watatu kushikililiwa na Polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi wa kiume.
Akizungumzia tukio hilo mwishoni mwa wiki, Mwalimu wa shule hiyo, Nicholaus Ulimwengu anayefundisha darasa la tano, alisema kuwa asubuhi alikuja Fatuma Ramadhan ambaye ni mzazi wa mtoto wa kike (8), na kudai kuwa mwanae huwa anachelewa kurudi nyumbani baada ya kutoka shule na huwa anakuwa na mwanafunzi mwenzake wa kiume (9).
Alisema kwa mujibu wa mzazi huyo, Oktoba 10 alimuuliza mwanae anakopita na kumwambia kuwa huwa wanaenda (anamtaja mwenzake wa kiume), na kufanya mapenzi kila siku.
“Sisi kama walimu ilibidi kuwauliza wanafunzi kama huwa wanafanya mchezo huo nao walikubali, ikabidi tuwaadhibu kwa kuwatandika viboko vinne kila mmoja ili wasirudie,” alisema mwalimu huyo.
Ulimwengu, aliongeza kuwa baada ya kuwaadhibu, mwanafunzi wa kiume alionekana kuwa na michubuko ya viboko kwenye makalio, kitendo kilichomfanya mzazi wake Mzee Ramadhan kwenda Polisi kuwashtaki walimu kwa kmjeruhi mwanae.
Mwanafunzi Shabani Kassimu anayesoma darasa la tano shuleni hapo, alisema kuwa wanafunzi hao walikuwa na tabia ya kuwa pamoja kila wakati wanapokuwa shule hata muda wa kutoka ila hawakujua wanakokuwa wakienda.
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Msaidizi (ACP), Japhari Muhamed, alithibitisha kushikiliwa walimu hao, Baraka Kilatunga (27), Jeje Msiba (32), na Michael Mugumwe (34), kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi.
Alisema kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani upelelezi wa awali utakapo kamilika.
October 22, 2014
Home
/
Unlabelled
/
MUNGU TUNUSURU..WANAFUNZI WA DARASA LA PILI WASHIKWA WAKIFANYA NGONO NI LIVE BILA CHENGA
MUNGU TUNUSURU..WANAFUNZI WA DARASA LA PILI WASHIKWA WAKIFANYA NGONO NI LIVE BILA CHENGA
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment