October 22, 2014

ROSE NDAUKA KUHAMISHIA PENZI KWA T.I..CHEK ALIVYOHAHAH USIKU WA FIESTA...

Katika hali ya kushangaza, staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka alinaswa akihaha kumtia kwenye himaya ya penzi lake Rapa kutoka Marekani, Clifford Joseph Harris ‘T.I’.
Rapa kutoka Marekani, Clifford Joseph Harris ‘T.I’.
Tukio hilo lililofuatiliwa hatua kwa hatua na mwanahabari wetu lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club wakati Mmarekani huyo alipokuwa akitumbuiza kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014.
Awali, Rose ambaye aliongozana na Mtangazaji wa Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’, mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ na mumewe, Gardner Dibibi, alisikika akiwaambia wenzake hao kuwa piga ua ataondoka na msanii huyo anayetamba na wimbo wa No Mediocre.

“Kama hamuamini mtaona, kifupi T.I ni shemeji yenu na hilo nitawaonyesha hapahapa pindi nitakapokaa naye,” alisikika Rose.
Kutokana na kuwalazimisha kwa muda mrefu wenzake hao wakubali wakiwa viwanjani hapo, ilifika wakati kila mmoja alikubaliana na hoja yake na kumuita ‘bebi’ wa T.I.
“Haya bwana, shem (T.I) anapanda saa ngapi?,” alisikika Gardner.
Staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.
Kama hiyo haitoshi, kuna wakati, Rose ambaye alionekana kama ulabu upo mahali pake, alitoweka katika kundi la wenzake kwa takriban dakika 20 akidai anakwenda nyuma ya jukwaa kumfuata T.I.

Hata hivyo baada ya muda alirejea na kudai imeshindikana kumuona kwa muda huo lakini atajitahidi hadi shoo itakapokwisha, atakuwa ameshakaa naye na kuzungumza naye kwa kirefu.
“Sijamuona ila hamna shida, nitamuona tu kabla shoo haijaisha,” alisikika Rose ambaye juzikati alimwagana na aliyekuwa mchumba’ke wa muda mrefu, Malick Bandawe.

Hadi mwanahabari wetu anaondoka viwanjani hapo, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake hakuwa amefanikiwa kumtia mikononi rapa huyo.

No comments:

Post a Comment