Ni shida! Mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’, hivi karibuni alimliza staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ baada ya kuchelewa kufika ukumbini akiwa MC (Master of Ceremony) kwenye shughuli ya mdogo wake (Davina).
Mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’.
Hata hivyo, nusu saa baadaye, Mai alitimba huku akimsindikiza bi harusi na kujitetea kuwa gari lake lilipata pancha barabarani.
Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’.
Baada ya Mai kuingia, Eva alimkabidhi ‘maiki’ kisha shughuli ikaendelea lakini baadaye ilionekana kuwa mkosi kwa Mai kwani shughuli ilipoisha, alilalamika kuibiwa redio ya gari lake ingawa haikujulikana kama iliibwa mahali hapo au alipopata pancha.Pamoja na yote, shughuli ilipendeza na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa mjini.
No comments:
Post a Comment