Msala! RB namba WH/RB/6335/2014-SHAMBULIO
LA KUDHURU MWILIkwenye Kituo cha Polisi cha Wazo Hill, Tegeta jijini Dar,
imemtia mbaroni mtangazaji maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu ‘Lady Hanifa’ na
mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Aneth kwa madai ya kutaka kumuua mhudumu
wa baa aliyetambulika kwa jina la Aika Andrew (32).
Mtangazaji maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu anayetuhumiwa kumshambuli mhudumu wa baa.
Uchunguzi wa gazeti hili
ulibaini kwamba sakata hilo la kusikitisha lilijiri wiki iliyopita kwenye baa
maarufu ya Shayo iliyopo Tegeta, Dar.Maelezo yaliyoandikishwa na Aika polisi
yalidai kwamba Lady Hanifa alifika kwenye baa hiyo ambayo ndani yake anamiliki
jiko la chakula na kuelezwa kwamba, siku moja kabla ya tukio hilo alikuwa na
deni na alipofika tu, Aika alimkumbushia ndipo balaa lilipoanza.
Ilisemekana kwamba Aika alimfuata na kumwambia kuwa jana yake alikuwa akidaiwa bia moja tu ya baridi aliyokuwa amekopa, kitendo kilichompandisha hasira na kuona kama amefedheheshwa kudaiwa mbele za watu
Ilidaiwa kwamba alimwita
mfanyakazi wake, Aneth ili ampatie fedha aliyokuwa akidai Aika lakini muda
huohuo Lady Hanifa akaanza kudai chenji yake kwa mabavu.
Ilidaiwa kwamba kulitokea majibizano makubwa ndipo mtangazaji huyo akaanza kumshambulia Aika huku akipewa sapoti na Aneth..
Ilidaiwa kwamba kulitokea majibizano makubwa ndipo mtangazaji huyo akaanza kumshambulia Aika huku akipewa sapoti na Aneth..
Iliendelea
kudaiwa kwamba katika purukushani hizo, Aneth aliyekuwa ameshika kisu alimchoma
nacho Aika tumboni, kichwani, mikononi huku Lady Hanifa akimuunguza
shingoni kwa kutumia upawa wa chipsi uliokuwa na mafuta ya moto kisha
wakakimbia.
Habari zilieleza
kwamba baada ya hapo Hanifa na Aneth walikimbilia Kituo cha Wazo Hill kutoa
taarifa lakini muda mfupi wasamaria wema walifika katika kituo hicho wakiwa na
Aika aliyekuwa ametapakaa damu mwili mzima.
Polisi waliwashikilia Lady Hanifa na Aneth na Aika akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.
Polisi waliwashikilia Lady Hanifa na Aneth na Aika akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.
No comments:
Post a Comment