Msanii wa muziki Ray C amedai hawezi toka kimapenzi tena na msanii
kutokana na kuumizwa na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Lord Eyes.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha ENewz cha East Africa Television
kuwa toka aachane na Lord Eyes hajawahi kuingia tena kwenye mahusiano na
kudai kuwa msanii huyo alimuumiza sana mpaka yeye kuingia kwenye
matumizi ya dawa za kulevya kipindi hicho.
“Kwa sasa bado sina boy friend, now nina marafiki tu kiukweli nafasi
hiyo bado maana Lord Eyes aliniumiza sana, nilimpenda sana na ndiyo
maana nilifanya alichokuwa akifanya, sikutegemea kama ingekuwa vile,
hata kwenye drugs unakutana na rafiki yako anafanya hiki na wewe utataka
kufanya ili aone upo naye pamoja, ila kwa sasa mimi na wasanii hapana,
ni bora hata nitoke na msukuma mkokoteni ili mradi anipende maana mimi
nina mapenzi ya kweli ndiyo maana unaona hata nyimbo zangu nyingi ni za
mapenzi” Alisema Ray C.
February 25, 2016
Home
/
Unlabelled
/
Kuliko Nitoke Kimapenzi na Msanii, ni Bora Hata Nitoke na Msukuma Mkokoteni – Ray C
Kuliko Nitoke Kimapenzi na Msanii, ni Bora Hata Nitoke na Msukuma Mkokoteni – Ray C
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment