Kwa wiki kadhaa kwenye kwenye mtandao wa Instagram kumekuwa na
majibishano ya vijembe kati na Wema Sepetu na Zari hasa kuhusiana na
uhalali wa mtoto wa Tiffah kama ni wa Diamond. Zari amepiga stori na
@cloudsfmtz moja kwa moja kutoka Sauz.
‘’Ngoja nikwambie kitu mimi ni mzazi ni muda mrefu Wema na timu yake
wamekuwa wakimsema mtoto wangu…Mara Oooh Tiffah Katunzi…Tiffah
Ivan..Sasa ninachoshangaa Wema hayupo na Diamond sasa mambo ya Tiffah
yanamuhusu nini? Haya hata kama mtoto ni mtoto wa hao watu wanaowataja
yeye na ‘team’ yake inawahusu nini?,’’Zari.
‘’Yeye sio familia ya Diamond amebaki kuwa ‘ex’ kama akina Jokate,Wolper
wote wametulia wanafanya mambo yao,kwanini Wema anatuma watu wamatukane
mtoto wangu kuwa angekuwa mzuri tungehama mjini,mara mtoto mwenyewe
mbaya,Zombi nimewavumilia sana ndio maana nikawajibu,’’Zari.
‘’Mbona wao wanafake maisha yao kuanzia magari,nyumba ,atafute kazi
afanye au a’promote’ lipstick zake ..’No need for DNA Tiffah ni wa
Diamond …Nimefunga mjadala,’’Zari.
No comments:
Post a Comment