Habari zinazosambaa kwa kasi ya ajabu kama moto wa kifuu zinaeleza kuwa,
mtoto mzuri ndani ya Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ mbali na taarifa
za kuwa mjamzito, hadi sasa bado yupo kwenye wakati mgumu kuweza
kutegua kitendawili cha nani mmiliki halali wa kiumbe kilichopo tumboni
mwake, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.
Hivi karibuni, magazeti tofauti ya Global Publishers ndiyo yalikuwa ya
kwanza kuripoti kuhusu uwepo wa mimba ya mlimbwende huyo asiyechuja
Bongo, ambapo awali, vyanzo mbalimbali vilieleza kuwa mhusika ni mbunge
mmoja machachari ambaye ndiye anayemuweka Wema mjini kwa sasa.
MAJIBU YA WEMA ALIPOBANWA
Kwenye habari ya awali iliyoripotiwa na gazeti la Ijumaa, Wema
alipotafutwa kusomewa mashitaka yake kuwa ana ujauzito wa mbunge huyo,
kupitia simu ya shosti wake, Aunt Ezekiel, staa huyo hakutaka kufunguka
sana kuhusu mbunge huyo zaidi ya kusema; “ndiyo nina mimba, tena ya
miezi sita.”
UBUYU MPYA SASA
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006
amejiridhisha kuwa ni mjamzito baada ya kupima kwenye hospitali moja
maarufu (jina tunalo) na kuondoka na furaha ya ajabu lakini kitendawili
alichoondoka nacho ni kuwa hamjui mhusika wa kiumbe hicho.
WOTE AWAPA ASILIMIA 50
“Madam alifurahi kweli maana suala lililokuwa linamnyima usingizi siku
zote ni kutopata mimba. Baada ya furaha hiyo, ishu ikawa ni kumtambua
mhusika kwani kwa nyakati tofauti ameshabanjuka kimalavidavi na mshindi
wa Big Brother Hot Shot 2014, Idris Sultan na mbunge yule anayempa jeuri
ya pesa kwa sasa, wote amewapa asilimia hamsini hajajua nani hasa ndiyo
mhusika,” kilisema chanzo hicho.
WOTE WAWILI KAWAMILIKISHA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, baada ya kuona ameshachanganya
madawa, Madam aliamua kila mmoja kumwambia kuwa ‘mzigo’ huo ni wake
hivyo wote kwa pamoja na nyakati tofauti wanahudumia na kumjali staa
huyo, tena kwa nguvu zote.
“Yaani kila mmoja kamwambia mimba yake. Wote wawili wamezipokea taarifa
za ujauzito kwa bashasha huku kila mmoja akijiamini kuwa ni mhusika
pasipo kujua Madam hajui nani hasa ndiye halisi.
MBUNGE, IDRISS ‘FULL’ KUHUDUMIA
“Yani ni full kuhudumia. Mbunge kwa wakati wake amekuwa akimwaga chapaa
kama hana akili nzuri. Amelipia nyumba ile ya Ununio jijini Dar na kama
hiyo haitoshi, amekuwa akisimamia shopping za maana tu mjini na hata ile
ndiga aliyojizawadia Wema katika sherehe yake ya kuzaliwa, mbunge huyo
alihusika katika malipo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Idris naye si haba. Anajitutumua kwa upande wake, anaamini kwamba mzigo ni wake bila kujua mimba hiyo ina figisufigisu.”
IDRIS ASAKWA, AFUNGUKA
Gazeti hili lilimtafuta Idris kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopokea, alitiririka hivi:
Risasi: Mzee tumepata habari kwamba wewe ndiyo mhusika wa mimba ya Madam, vipi unazungumziaje taarifa hizo?
Idris: Kwenye hilo kwa sasa siwezi kuliongelea, labda unipe mwezi mmoja. Kichwa changu hakijatulia.
Risasi: Lakini inasemekana unagharamia kila kitu kwa sasa, ukiamini mzigo ni wako?
Idris: Aaa! Acha kuniingizia hayo mambo bwana. Wewe subiri huo mwezi mmoja ukipita nitakueleza kila kitu.
SHOGA ZAKE WAMSHANGAA!
Mashosti wake waliozungumza na Gazeti hili ambao hawakutaka kutajwa
majina yao, walisema ni jambo la kushangaza kwa mwanamke kushindwa
kumjua mwanaume aliyempa ujauzito.
WEMA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za kutosha kumsaka Wema kwa kumpigia simu
na kumtumia ujumbe mfupi lakini hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
KUTOKA KWA MHARIRI
Mimba ni jambo la kheri hivyo kwa kuwa Wema ameziona simu za wanahabari
wetu zikimuuliza juu ya mhusika wa kiumbe hicho, ni vyema akawapigia na
kuanika kila kitu kuhusu habari hii.
CHANZO: Global Publishers (GPL)
January 15, 2016
Home
/
Unlabelled
/
TETESI za Ujauzito wa Wema Sepetu Zawa Gumzo, Yadaiwa Hamjui Mwenye Mimba Hiyo Kama ni Idriss ama Mbunge
TETESI za Ujauzito wa Wema Sepetu Zawa Gumzo, Yadaiwa Hamjui Mwenye Mimba Hiyo Kama ni Idriss ama Mbunge
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment