Nuh Mziwanda amedai kuwa aliyofanyiwa na Shilole ni mengi
na mazito ambayo ilibidi ayafiche kwa maslahi ya penzi lao na heshima
kwake
Akiongea kwenye kipindi cha D’Weekend Chat Show cha Clouds
TV Ijumaa hii mbele ya Shilole aliyekuwa amejikunyata pembeni kwa
kukasirishwa na uwepo wa ex wake studioni hapo bila kutaarifiwa
mwanzoni, Nuh alisema Shilole hakuwa mwanamke wa kutawaliwa.
“Yeye anajua mambo gani alikuwa anafanya kwangu mambo
ambayo yalikuwa hayastahili anifanyie. Alikuwa anafanya kwa kunichukulia
poa kwamba nitafanya nini lakini at end of the day kila kitu kina
mwanzo na mwisho,” alisema.
Nuh alisema ni ngumu tena kurudisha imani kwa mpenzi wako
huyo licha ya kukiri kuwa bado hajaweza kuwa tayari kuwa na mwanamke
mwingine kwa sasa.
No comments:
Post a Comment