Mh.Paul Makonda akizungumza na Clouds Fm katika kipindi cha
Jahazi anasema tarehe 5/1/2016 ujenzi wa shule 7 katika wilaya ya
kinondoni ulianza na amezindua kampeni ya kuchangia ujenzi wa shule Saba
za kata katika wilaya ya Kinondoni ili kupunguza upungufu wa shule
katika wilaya hio ambapo zitachukua zaidi ya vijana 3183
Akiongelea maendeleo ya Kampeni hio amesema inaenda vizuri na michango inaendelea kumfikia na witikio umekuwa mkubwa sana!
Akitoa tathimini fupi amesema amepokea Mifuko 500 ya cement
toka kwa Dr mwaka....mifuko 1000 ya cement toka kwa watu mbalimbali na
umoja wa mafundi geleji wametoa mifuko 50 ya cement! Amesema ameamua
kujenga shule hizo saba kuondokana na tatizo la upungufu wa shule katika
wilaya ya kinondoni na kuongeza kuwa Elimu ni njia bora na pekee ya
kuwapa urithi wadogo zetu na watoto zetu! Ameendelea kuwaomba wadau
wengine kuendelea kujitokeza kuchangia kwani Kutoa ni moyo na si utajiri
ameomba mwenye chochote hata mfuko mmoja wa simenti iwe hata tofari
moja au mawe na mchanga wanapokea chochote
MAONI YANGU!
Mh.Paul Makonda ni mfano wa kuigwa kwa wakuu wa mikoa na
wilaya zote hapa nchini katika utendaji wa kazi,Hata wabunge pia ni
lazima wajifunze toka kwa Makonda na si kubaki kuilalamikia serikali
inafanya nini ni wakati wa wao pia kusema serikali wameifanyia nini
Ukiacha maneno yanayo semwa kuhusu Mh.Paul Makonda utendaji
wake wa kazi wananchi wengu wameupenda pamoja na mapungufu machache
alio nayo
No comments:
Post a Comment