Hamida Hassan
Ule msemo kwamba duniani ni
wawiliwawili umeonekana kuwa na nguvu baada ya kuwepo kwa binti mrembo
anayefanana sana na staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Binti
huyo anayefahamika kwa jina la Tuerney ambaye pia ana shepu bomba,
amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram na Facebook
kwani wadau wamekuwa wakiweka picha zake na za Wema kisha kuonesha jinsi
walivyofanana.
Ijumaa lilifanya
jitihada za kutaka kumjua kwa undani lakini katika kuonesha si mtu wa
kutaka umaarufu kivile, alipotafutwa alikataa kutoa ushirikiano akisema
yeye hataki mambo ya magazeti. Jionee picha!
No comments:
Post a Comment