WATU wawili wamefariki dunia Papo hapo baada ya Gari walilokuwa wakisafiria lililobeba Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kwenda mkoani mkoani Mbeya kupata ajali Eneo la Kitonga Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Ajali
hiyo imetokea leo alfajiri baada ya dereva wa Gari hilo kujinusuru
kugongana uso kwa uso na gari jingine, hivyo kulazimika kuingia nyuma ya
lori na kupelekea kifo chao.
Kwa
mujibu wa Wakala Afisa mauzo wa magazeti ya Mwananchi Mkoa wa Iringa
Alex Kadea ambae alifika Eneo la tukio ameithibitisha kutokea kwa ajari
hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa matukiodaima kuwa waliofariki dunia wote wawili walikuwa ni madereva wa Gari hilo.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment