Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameanza ziara mkoani Kigoma huku akiahidi
kuanza ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya viwango vya ‘standard gauge’,
itakayosaidia kuimarisha biashara ya kusafirisha mizigo kutoka Dar es
Salaam kwenda nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC),
kupitia Bandari ya Kigoma.
Tamko la Waziri Mkuu Majaliwa inaashiria kuanza kwa utekelezaji wa
vipaumbele 25, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati, alivyovitoa Rais John
Magufuli (wakati huo akiwa mgombea urais wa CCM), Agosti 24, wakati wa
uzinduzi wa kampeni zake kwenye Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na wakazi wa Kigoma katika Mwalo wa Kibirizi, Waziri Mkuu
Majaliwa alisema mradi huo utaambatana na ujenzi wa bandari kavu eneo la
Katosho mjini Kigoma, kwa ajili ya kushusha mizigo inayosubiri kwenda
nje ya nchi.
“Lazima tujenge reli ya kisasa na tumezindua ujenzi wa reli ya urefu wa
kilomita mbili. Huwezi kuimarisha bandari kama reli itakuwa imechoka na
hii ilijengwa miaka 100 iliyopita, sasa imezeeka haifai, ndiyo maana
tumeamua kutumia fedha nyingi kuhakikisha mradi huu wa reli ya kisasa na
ujenzi wa bandari unakamilika kwa wakati,” alisema Waziri Mkuu
Majaliwa.
Katika maelezo yake hayo Majaliwa alipokea kilio cha wakazi wa Katosho
inakotakiwa kujengwa bandari kavu wanaolalamika kupunjwa malipo ya fidia
ya nyumba na mazao, aliwahakikishia kuwa mchakato wa kutathmini
unarudiwa hivyo aliwashauri wananchi waliopokea fedha za fidia kuhama
ili kupisha ujenzi wa bandari.
Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wavuvi na wafanyabiashara kutumia fursa
ya Mwalo wa Kibirizi, ambalo linapokea mazao ya uvuvi na kuyachakata kwa
ajili ya kuingia sokoni, jambo litakalosaidia kuinua uchumi na kuongeza
thamani ya mazao hayo.
Alisema Serikali itatafuta masoko ndani na nje ya nchi kwa ajili ya
kuuza samaki na dagaa wanaovuliwa kutoka Ziwa Tanganyika na kuwezesha
wavuvi kujiongezea kipato, hali itakayowafanya wawe na uwezo wa kununua
zana bora za uvuvi na kuongeza kiwango cha uvuvi.
Pia aliahidi kumuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali
wa Polisi (IGP), Ernest Mangu kuongeza ulinzi Ziwa Tanganyika ili
kupambana na maharamia wanaopora zana za uvuvi, ambapo pia amemuagiza
mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya kufanya kikao na Balozi wa Congo
DRC ili kuona njia bora ya kushirikiana kupambana na maharamia.
December 30, 2015
Ahadi ya Rais John Pombe Magufuli ya Ujenzi wa Reli Kuanza
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment