Haruni Sanchawa
SIMANZI, vilio na huzuni vimetawala nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila mara tu baada ya familia yake kupokea taarifa za kifo chake kilichotokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani baada ya gari waliyokuwa wakisafiria aina ya Toyota GX 100 kupata ajali.

Mke wa Mtikila akilia kwa uchungu.
Taarifa za ajali hiyo zilipatikana saa 11.15 alfajiri, wakati kiongozi huyo akiwa na wenzake wakitoka mkoani Morogoro.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, nyumbani kwa Mtikila Mikocheni, Dar, jana, Katibu Mwenezi wa Chama cha DP, Sambichaka Feruzi alisema:
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, nyumbani kwa Mtikila Mikocheni, Dar, jana, Katibu Mwenezi wa Chama cha DP, Sambichaka Feruzi alisema:
“Mtikila aliondoka Dar Ijumaa jioni na watu kadhaa kulekea mkoani Njombe kwa shughuli za kichama kwa ajili ya kumfanyia kampeni mgombea ubunge Jimbo la Njombe Mjini, Nicodemas Ngwala kupitia Chama cha DP ambapo shughuli hiyo ilimalizika juzi jioni na kiongozi huyo kuanza safari ya kurejea Dar kwa shuguli zingine za kichama.”
....Akibembelezwa.
Sambichaka alielezea namna ambavyo wao walipata taarifa ya ajali hiyo kutoka mmoja wa watu waliokuwa kwenye msafara huo aliyemtaja kwa jina moja la Mgaya baada ya kupiga simu na kusema kuwa wamepata ajali maeneo hayo na kudai kuwa watu watatu waliumia huku Mtikala akifariki dunia.
Marehemu Mtikila enzi za uhai wake.
Baada ya ajali hiyo majeruhi walipelekwa katika Hospitali ya Tumbi kisha mwili huo uliamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbi.Hata hivyo, vilio, majonzi na simanzi vilitawala zaidi kwa waliohudhuria nyumbani kwa marehemu hasa pale mke wa marehemu, Georgia Mtikila alipokuwa akisikika akilia: “Darling has gone, Mungu nifanyeje nimebaki mwenyewe.’’
No comments:
Post a Comment