October 5, 2015

MREMBO ANASWA AKIIBA SUPERMARKET

Imelda mtema
Ni aibu 100%! Mrembo mkali aliyetambuliwa kwa jina moja la Winifrida, amekumbwa na fedheha ya aina yake baada ya kunaswa akiiba pafyumu kwenye supermarket ikidaiwa kuwa tabia hiyo kwa sasa imeshamiri jijini Dar kwa mabinti walio wengi.

Mrembo huyo akidhibitiwa.
Tukio hilo la aibu ya kupitiliza lililonaswa na gazeti hili lilijiri wikiendi iliyopita ndani Supermarket ya TSN iliyopo maeno ya Bamaga-Mwenge jijini Dar.Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, mrembo huyo aliingia kwenye supermarket hiyo akiwa amebeba pochi kubwa huku akiwa anazunguka na kuangalia bei ya vitu na alipofika katika shelfu la pafyumu alisimama hapo.
...Akificha sura yake kwa aibu.
Shuhuda huyo alisema kuwa baada ya kuona mrembo huyo amesimama hapo kwa muda mrefu wahudumu walianza kumpiga chabo ambapo waligundua anachukua pafyumu hizo na kuziweka kwenye mkoba wake huku akiwa amejiziba na pampers ya mtoto aliyoishika akiangalia bei.
“Nilimuona anavyochikichia zile pafyumu lakini nikamnyamazia tu kwa sababu nilitaka nione mwisho wake ni nini.
“Nilimuacha hadi alivyozoa nyingi na akaanza kuondoka,” alisema shuhuda huyo.
Baadhi ya vitu alivyoiba.
Mpashaji huyo alisema kuwa baada ya kujaza mkoba, mrembo huyo aliamua kuondoka ndipo wafanyakazi hao wakamfuata nje na kumwambia arudi ndani kabla ya kumuaibisha.“Baada ya kurudi, baadhi ya watu walianza kumpa kichapo kwani mara kwa mara wafanyakazi wanakatwa mishahara kutokana na upotevu wa vitu,” alisema shuhuda huyo.
Alisema kuwa, baada ya kichapo hicho, mrembo huyo alipelekwa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ ambapo alitakiwa kulipa mara mbili ya gharama ya vitu vyote alivyokutwa navyo. Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, mrembo huyo alikuwa kwenye harakati za kulipa vitu hivyo.

No comments:

Post a Comment