October 15, 2015

MWILI WA WAZIRI KIGODA WAWASILI DAR KUTOKA INDIA


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, enzi za uhai wake.Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akijumuika na Watanzania wengine kuupokea mwili wa marehemu Kigoda.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli naye yupo kuungana na Watanzania wengine kuupokea mwili wa Kigoda.Ndugu, Jamaa na marafiki wakiusubiri kuupokea mwili wa Kigoda.....Hudhuni ikitawala.Ndugu, Jamaa na marafiki wakiusubiri kuupokea mwili.Hali ya majonzi ikitawala eneo loa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere Dar.
Mwili wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda aliyefariki juzi katika hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu, umewasili leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Emirates.
Mwili wa Waziri Kigoda utaagwa kesho viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

VIDEO YA TUKIO

No comments:

Post a Comment