October 19, 2015

MAGUFULI AITIKISA MWANZA, HAIJAWAHI TOKEA!

mshakaji akipiga push up wakati msafara ukipita
Njemba mmoja akipiga push up wakati msafara wa Dk Magufuli ukipita.mdada akimfagilia njia magufuli
Dada akimfagilia njia MagufuliAfande akimtoa barabarani mdada aliyekuwa akifagia barabara ili magufuli apite pakiwa safi
Afande akimtoa barabarani mdada aliyekuwa akifagia barabara ili Magufuli apite pakiwa safi.magufuli akimwaga sera
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli akimwaga sera kwa wakazi wa Mwanza katika Viwanja vya Furahisha jijini humo jana.
watoa huduma ya kwanza walikuwa na kazi ya ziada ya kuwaokoa waliobanwa na kupoteza fahamu
Kutokana na msongamano mkubwa wa watu mdada huyu alikosa hewa na kuzirai.Temba 'kushoto' na Chegge wakikamua
Chege na Temba wakifanya yao jukwaani.sehemu ya umati uliofurika uwanjani hapo
Umati wa watu waliofika katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jana wakimsikiliza Dk Magufuli.
jamaa wakiwa kwenye Tingatinga ambalo linawakilisha alilopewa magufuli kwaajili ya kazi zake za umahiri
Jamaa wakiwa kwenye Tingatinga ambalo linaashiria jina alilopewa Magufuli "Tingatinga" kwa umahiri wake wa utendaji kazi.bibi huyu ni miongoni mwa umati mkubwa wa watu waliozikubali sera za magufuli
Bibi huyu ni miongoni mwa umati mkubwa wa watu waliozikubari sera za Magufuli.
kutokana na msongamano mkubwa wa watu mdada huyu alikosa hewa na kuzimia-001
Baada ya kukoswa hewa dada huyu naye alidondoka, watu wa huduma ya kwanza wakimsaidia.
 
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli jana alifanya kufuru na pengine kuvunja rekodi ya mgombea urais aliyewahi kufanyiwa mapokezi makubwa na wananchi mkoani hapa (Mwanza).
Magufuli alitua kwenye uwanja wa ndege wa jijini hapa na kupokelewa na umati mkubwa wa watu ambapo baada ya kuanza kuelekea Viwanja vya Furahisha kufanya mkutano wa kampeni za kuomba ridhaa kwa wananzchi, alilazimika kusimama njiani vituo kadhaa kutokana na kuzuiwa njiani na wananchi hao waliokuwa na shauku na kuongea nae na kusikiliza sera zake.
Akielekea viwanja vya Furahisha aliopoandaliwa jukwaa la kumwaga sera zake, Magufuli alilazimika kusimama maeneo ya Pasiansi, Nyamanoro, Kitangiri, Kona ya Bwiru ndipo akafika Viwanja vya Furahisha na kukuta nyomi la watu lililokuwa likimsubili.
Akiwa kwenye mkutano huo Magufuli aliwahidi wakazi hao serikali yake kununua meli mbili mpya na kubwa kwa ajili ya kutoa huduma kati ya Mwanza, Bukoba na Musoma.
Magufuli pia aliwahidi wakazi hao kuwatengenezea reli ya 'standard gauge' itayoweza kuhimili mabehewa yenye mizigo mizito ambayo itakuwa kati ya Mwanza, Kigoma, Tabora, Mpanda mpaka Dar.
Magufuli aliwahidi wakazi hao kuwajengea daraja kubwa likakalounganisha kivuko cha Kigongo na Busisi ili watu na magari yapite yenyewe. Magaufuli aliwahidi wakazi hao kuifanya mwanza kuwa jiji la kibiashara na kuwa Geneva ya Afrika.

No comments:

Post a Comment