October 2, 2015

HAMISA MOBETO: Ndoa yangu Itazinduliwa Mtandaoni.....

Imelda Mtema
Mwanamitindo Hamisa Hassan ‘Mobeto’ amefunguka kuwa siku atakayofunga ndoa atafanya siri na watu wataiona kwa mara ya kwanza kupitia mitandao ya kijamii.


Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Hamisa alisema kuwa ndoa yake itakuwa ya siri kwa maana atafunga na mumewe Kiislamu bila kuita watu na picha za ndoa hiyo zitazinduliwa mtandaoni.

“Watu wakishaziona picha hizo kupitia mitandao ya kijamii ndiyo nitafanya pati ya kusherehekea, nataka kwangu kiwe kitu cha tofauti kidogo,” alisema Hamisa ambaye ni mama wa mtoto mmoja.
Source:GPL

No comments:

Post a Comment