October 2, 2015

ESMA PLATNUMZ: Namshangaa Sana Diamond Kuwa na Chuki Kiasi Hicho Kwa Baba Yake Mzazi


Brighton Masalu
DADA wa ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma amemshangaa kaka yake, (Diamond) kwa kuendeleza chuki dhidi ya baba yake mzazi, mzee Abdul Jumaa.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu hivi karibuni, Esma alisema siku zote si vyema kukaa na kinyongo au chuki dhidi ya wazazi na hata kama ikitokea ni vyema kuyamaliza kwa mtoto kujishusha.

Hata mimi nilishawahi kukosana na baba yangu, lakini nilishasamehe na kusahau kabisa, hata hapa nyumbani, ni mara nyingi tu huwa tunatofautiana na mama lakini hata kama yeye kakosea, huwa najishusha si kama ilivyo kwa Nasibu (Diamond) kuwa na chuki kali kiasi hicho dhidi ya baba yake,” alisema Esma.

Source:GPL

No comments:

Post a Comment