BREAKING NEWS: Mwanasiasa mkongwe ambaye ni kada maarufu wa chama cha CCM Ndugu Kingunge Ngombale Mwiru ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama hicho cha siasa na amesema sababu kubwa ni kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa chama hicho kwa sasa.
Amesema hatojiunga na chama kingine cha siasa ila anaamini vijana, kinamama, na watanzania wanahitaji mabadiliko na yeye yuko upande wa mabadiliko.
No comments:
Post a Comment