October 05 2015 ni siku ya pili inaisha
tangu litokee tukio la ajali ya gari ndogo katika Kijiji cha Msolwa,
Chalinze Mkoa wa Pwani ambapo ndani yake kulikuwa na watu watatu pamoja
na Mwanasiasa Mkongwe Tanzania, Mchungaji Christopher Mtikila ambaye alifariki kutokana na ajali hiyo.
Tangu kutokea kwa ajali hiyo mambo mengi
yameongelewa kuhusu ajali na kifo chake, mazingira ya ajali? Marehemu
kutokuwa na jeraha? Mchungaji kufariki na wengine kupona? Ripoti ya
Hospitali? Mazishi?
Familia ya Mchungaji Mtikila imeweka kila kitu sawa >>>> “Mchungaji Christopher Mtikila
alipata ajali majira ya saa 11 Alfajiri eneo la Msolwa Chalinze, bahati
mbaya alikuwa hajafunga mkanda na gari ilikuwa speed… Kulikuwa na gari
llilikuwa lime-overtake upande wao, dereva wao akakwepa kwenda kushoto“.– Victor James Manyai, Msemaji wa Familia.
Hapa Msemaji wa Familia anasimulia mazingira ya ajali ilivyokuwa >>> “Eneo
lile barabara imeinuliwa juu zaidi na eneo la pembeni limeshuka chini..
gari lilipaa juu, liliposhuka chini matairi yakapasuka yote, kwa sababu
hakuwa amevaa mkanda akatokea mbele ya kioo cha gari.. alipoenda
kuangukia, gari likaenda kumfunika upande wa kushoto, akawa hawezi
kupumua“.- Victor Manyai.
Watu wengine walitoka na Majeraha kwenye gari, nini kilifanya Mchungaji afariki pekeyake? >>> “Ilichukua
muda kwa sababu walikuwa watu wanne, mmoja alikuwa ameumia zaidi,
mwingine alitupwa mbali… ilibidi mpaka wasamalia wema waje kusaidia
kumuinua… walijaribu kumsaidia lakini hakuweza kupumua tena“.
Kuna stori kwenye Mitandao ya Kijamii kuhusu kifo chake huku wengine wakihoji kwa nini mwili wa Mchungaji Mtikila haujaonekana kuwa na majeraha yoyote? >>> “Mimi
nilikuwepo katika Kikosi cha watu waliofanya postmortem pale Kibaha,
tulikuwa na madaktari wanne, madaktari wawili wa Familia, mmoja wa
Polisi na mmoja wa Hospitali ya Kibaha… sio kweli kwamba hana majeraha,
alikuwa na majeraha kichwani na miguuni, ila siwezi kutaja siri za
Marehemu ni kinyume cha maadili... Ukweli ni kwamba alikosa hewa, na kama kungekuwa na msaada wa dharura maisha yake yangeokolewa…“>>>
Gari alilopata nalo ajali je? >>> “Ukweli
ni kwamba gari lilikuwa limekodiwa, Mchungaji alikuwa na magari mawili
na yote yalikuwa katika Kampeni Mkoa wa Mara na jingine Wilaya ya
Kahama… Mimi ndio nilimkodia gari kwa madereva wa Taxi Mbezi mwisho, ni
vijana ambao nawafahamu.” >>>
Hii ndio Taarifa ya Familia kuhusu taratibu za kuaga Mwili wa marehemu na Mazishi >>> “Mwili
wa Marehemu kwa sasa upo Hospitali ya Lugalo, Jumatano tutaaga mwili wa
Marehemu Karimjee au Leaders Club, baada ya hapo tutasafirisha mwili
kwenda Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe” >>> Victor James Manyai, Msemaji wa Familia ya Marehemu Mchungaji Mtikila.
#RIP Mchungaji Christopher Reuben Mtikila.
No comments:
Post a Comment