September 14, 2015

Zitto: Hakika CHADEMA Watamkumbuka Dr. Slaa Baada ya Uchaguzi

Jana katika mahojiano na Tiddo Muhando kwenye kipindi cha Funguka, Zitto Kabwe amewaonya wana CHADEMA wanaomtusi Dr Slaa kwa sababu ya Lowassa kuwa watamkumbuka baada ya uchaguzi. Watu makini kama Dr Slaa na Prof Lipumba wanaondoka na watu eti wanamuona Lowassa leo kawa bora?


Zitto kasema hivi sasa CHADEMA msingi wake umekuwa ni "Lowassa" na si kupambana na ufisadi tena. Baada ya uchaguzi hakutakuwa na CHADEMA ile tuliyoifahamu na ndipo hapo watanzania watakapomkumbuka Dr Slaa.

No comments:

Post a Comment