September 10, 2015

Tahadhari Kwa Waumini wa Askofu Gwajima !

Ni muda mrefu jamii yetu imekuwa ikiwaheshimu na kuwaamini viongozi wa dini katika masuala mbalimbali ya kiroho na ustawi wa familia.

Ni jambo la kawaida sana kwa waumini wa dini zote kupeleka matatizo yao mbalimbali ya kifamilia kwa viongozi wa dini.

Ni dhahiri kwamba wengi wetu hupeleka masuala mbalimbali hata yale ya unyumba na siri nzito nzito za chumbani na familia kwa ujumla kwa kuwa tuna imani viongozi wa dini wana hulka ya kutunza siri na kusaidia kutatua matatizo yetu ya kiroho au kifamilia.


Hii ni tofauti kwa Gwajima ambaye ni mtomvu wa heshima ya kiongozi wa dini kwa kueleza siri za familia aliyoipa huduma za kiroho kisa tu kachokozwa kisiasa na yeye kajibu kwa kutoa siri za familia ya Slaa.

Angekuwa daktari angeweza kufutiwa cheti na kudaiwa fidia.

Lakini tukumbuke ni Gwajima huyu huyu aliyeshutumiwa kuvuruga ndoa ya Mbasha badala ya kutatua mgogoro wa familia hiyo.

Hii ni trend ya Gwajima anayejiita Bishop ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la Tahadhari hasa hasa na waumini wake wanaompelekea siri za ndani.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANI!!

By Jingalao/Jamii Forums

No comments:

Post a Comment