Dustan Shekidele, Moro
KATIKA hali isiyo ya kawaida wananchi mkoani hapa wamejikuta wakipigwa butwaa mara baada ya kumshuhudia staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba akivuta ‘mambo’ (shisha) kisha ‘kuzima gari’ ukumbini.
TUJIUNGE ENEO LA TUKIO
Tukio hilo lililopigwa chabo na mwanahabari wetu lilijiri mishale ya saa 8:00 usiku wa Jumamosi iliyopita katika ukumbi wa kisasa wa burudani wa Samaki Sport mjini hapa ambao kulikuwa na nyomi la kufa mtu.
Awali, baadhi ya wananchi walimpiga chabo Kiba kisha kumtonya paparazi wetu ambaye alifika fasta ndani ya kiwanja hicho na kumshuhudia laivu msanii huyo akiwa na demu mwingine mkali aliyejitambulisha kwa jina la Asia Mujuni na siyo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye amekuwa akifuatana naye kila sehemu katika siku za hivi karibuni.
JOKATE UPO?
Baadhi ya watu wanajua uhusiano wa Kiba na Jokate walidai kuwa kama mwanadada huyo angekuwepo eneo la tukio pangechimbika.
WAVUTA KWA ‘KUSHEA’
Wawili hao walikuwa wakivuta shisha kwa ‘kushea’ huku Asia akishushia na kinywaji kikali.
Hata hivyo, Kiba awali hakumgundua paparazi wetu hadi alipotonywa na msanii mwenzake, Stanley Yusuf ‘Stan Bakora’ ambaye anamfahamu fika mwandishi wetu.
Kiba aliyeonyesha kama amezidiwa nguvu kwa kilevi hicho, baada ya kutonywa alishtuka kisha akamchukua ‘patna’ wake huyo na kujikokota hadi kwenye gari ambapo walitokomea kusikojulikana.
MASTAA WENGINE WALIOKUWEPO
Kabla ya kutimua, kwenye meza aliyokaa Kiba na mrembo pia kulikuwa na wasanii wengine kama Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Esterlina Sanga ‘Linah’ na Kibwana Saleh ‘KB’ ambaye maskani yake ni mjini hapa.
Akizungumza na gazeti hili, KB ambaye pia alikuwa akivuta shisha alimtetea Kiba: “Kiba ni ndugu yangu na haya siyo madawa, ni shisha, Ulaya mastaa wanavuta. Baadhi ya watu humu ukumbini wanadai ni madawa ya kulevya lakini siyo kweli huu ni moshi wa kawaida.”
Naye mmoja wa mashabiki wa Kiba, Jumanne Idd aliyezungumza na gazeti hili kuhusu ishu hiyo alifunguka: ”Kila siku tunakuja kwenye kiwanja hiki cha Samaki, hatujaona watu wakivuta shisha humu ukumbini. Leo ndiyo tumemshuhudia Kiba kufuatia moshi wa kilevi hicho kuwa mkali, ilibidi mimi na demu wangu tuhame meza.”
Kijana mmoja wa mjini aliyefahamika kwa jina la Juma lssa alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema: “Ni kweli kifaa kile ni moshi wa kawaida lakini kuna baadhi ya watu wanachanganya na moshi wa bangi.”
KIBA ATAFUTWA
Jitihada za kumtafuta Kiba ili kuzungumzia ishu hiyo ziligonga mwamba na hata alipotafutwa kwa njia ya simu haikuwa hewani.
Shisha ni kiburudisho ambacho kimekuwa maarufu sana miongoni mwa mastaa na vijana wengine wa daraja la kati ambao hukitumia, hasa sehemu za starehe nyakati za usiku na mikusanyiko mingine ya burudani inayojumuisha watu wengi.
Source:Globalpublishers
September 10, 2015
Ali Kiba Avuta Mambo Mazito...Yamzidi na Kuzimia
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment