September 15, 2015

SHOGA: MADOIDO MUHIMU KWENYE ENEO LENU LA KUJIDAI!

Shoga yangu, leo nitazu-ngumza nawe mada iliyobebwa na kichwa hicho hapo juu.Bila shaka unaelewa ili kila kitu kiende sawa lazima kiwe na madoido yake, mfano ukitaka usifiwe kwa mapishi matamu lazima uweke viungo mbalimbali kwenye mapishi yako.
Ukitaka nyumba yako ipendeze lazima uipambe kwa mapambo mbalimbali, hata ukitaka kuonekana smati lazima ujue namna ya kupangilia mavazi yako.
Tukitoka kwenye mambo hayo, tukirejea kwenye eneo lako la kujidai lazima mwanamke uliyekubali kuolewa na kuwaacha wazazi na ndugu zako unapaswa kuwa na madoido ambayo yatamfanya mumeo asikinaike kuwa nawe.
Shoga, nasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya wenzetu licha ya kuwa hodari wa mapishi, kuwafanya waume zao waonekane maridadi muda wote lakini unapowarudisha kwenye tasnia ya yale mambo yetu ni ziro kabisa.

Wenzetu hao, hawajui namna ya kuwapagawisha waume zao kwa kuwadekea, kuwachanulia tabasamu na kuwalilia pia.
Shoga, hivi hujui kama kumdekea, kuachia tabasamu pana na kumlilia mumeo mnapokuwa eneo lenu la kujidai ndiko kumpagawisha kwenyewe?
Hivi hujui kama hao michepuko wa nje huwashika waume za watu kwa kuwafanyia hivyo na wengine wapokuwa eneo la kujidai hulia mwanzo mwisho hata kama ni uongo ili amteke akili?Mwisho wa kupeana makesheshe hata akimuomba mumeo shilingi milioni moja jamaa atakwenda kumchukulia benki na kumkabidhi kisha kumuuliza anataka nini kingine!
Kama hukuwa na utamaduni wa kumdekea, kuangua kilio cha ushirikiano wakati mnanesanesa kwenye dimba la chumbani anza leo shoga yangu vinginevyo wanaojua kulia na kudeka watamchukua mumeo jumla.
Kumbuka hata Yamoto Band wametoa kibao kinachoitwa Cheza kwa Madoido. Bye.

No comments:

Post a Comment