Staa wa muziki Bongo, Rehema Chalamila `Ray C’.
Mayasa Mariwata
Yamekuwa hayo tena! Staa wa muziki Bongo, Rehema Chalamila `Ray C’ yupo kwenye hofu nzito ya kutaka kuuawa kwa kile alichodai ni chuki za binadamu wasiomtakia mema.
Yamekuwa hayo tena! Staa wa muziki Bongo, Rehema Chalamila `Ray C’ yupo kwenye hofu nzito ya kutaka kuuawa kwa kile alichodai ni chuki za binadamu wasiomtakia mema.
Wikiendi iliyopita Ray C alitupia ujumbe mzito mtandaoni uliosomeka: “Nacheka lakini sina furaha ila najua kabisa mpango wao kwangu ni kuniua kabisa nipotee! Sitakufa bali nitaishi! Nashukuru kuwa ninajua haki yangu!
“Ndiyo chanzo chote cha chuki na fitina! Ila kumbukeni na ninyi mna watoto pia muombeni Mungu awaepushie hili balaa ndani ya familia zenu ila kumbukeni tu kuwa malipo ni hapahapa duniani tena siku wala si nyingi.”
Ilielezwa kwamba, Ray C alitoa ujumbe huyo akiwalalamikia watu ambao wamekuwa wakimnyima dozi ya Methadone ya kuondoa sumu ya madawa ya kulevya mwilini.Akichati na gazeti hili, Ray C alisema hiyo yote ni mtihani tu kwa binadamu.
Views: 177
No comments:
Post a Comment