Mark James Mwandosya |
Baada ya kuendelea kuzagaa kwa taarifa hizo nimeamua kufanya uchunguzi wangu binafsi dhidi ya madai hayo lakini nilichoambiwa na mmoja kati ya watu wa karibu sana wa Prof.Mwandosya na familia yake ameniambia kuwa PROFESA mara kadhaa amekuwa akihojiwa na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wanachama na makada waandamizi wa chama amekuwa akijibu na kusisitiza kuwa HANA MPANGO WA KUHAMA CCM.
Aidha duru za udadisi zinaeleza kuwa PROFESA kwa sasa yupo nchini MAREKANI katika shughuli zake binafsi.
Kwa kuwa wakati ni ukuta nadhani tusubiri tuone ataamua nini, kwenda kujivua nguo upinzani kama SUMAYE na mwenzie LOWASSA au ataendelea kulinda heshima na utu wake akiwa ndani ya CCM.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU BARIKI UCHAGUZI
MUNGU MUONGEZE PROFESA MWANDOSYA KATIKA KUTOA MAAMUZI YAKE
AMEN.
By Kawakama
No comments:
Post a Comment